Serikali imejiandaa kuleta Muswada wa Sheria bungeni kutoa haki ya
kusoma kwa watoto wote wa kike na kiume wa shule za msingi, sekondari na
kutoruhusiwa kuoa au kuolewa.
Aidha, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema
serikali inaendelea kukamilisha utaratibu wa kupata maoni ya wananchi
kuhusu marekebisho ya Sheria ya Ndoa na kutungwa kwa Sheria mpya ya
Mirathi na Urithi kuondokana na mkanganyiko uliopo kuhusu sheria hiyo.
Bunge lilielezwa hayo jana mjini Dodoma wakati waziri huyo akijibu swali
la nyongeza la Mbunge wa Ileje, Janeth Mbene (CCM) aliyehoji ni lini
serikali itaanza maandalizi ya kuchukua maoni juu ya kufanya marekebisho
sheria ya ndoa ya mwaka 1971.
Akijibu swali hilo, Dk Mwakyembe alisema hatua za awali zimeshaanza
kuchukuliwa na wizara hiyo ili kupata maoni ya wananchi juu ya
marekebisho ya sheria hiyo ya ndoa ya mwaka 1971 na kutungwa kwa sheria
mpya ya mirathi na urithi.
Alisema serikali ina nia ya dhati ya kufanyia marekebisho sheria ya ndoa
na kwamba mchakato huo ulisitishwa kwa kuwa Tume ya mabadiliko ya
Katiba ilikuwa ikikusanya maoni kuhusu mabadiliko ya katiba , hivyo
walidhani wananchi wangetoa pia maoni juu ya sheria hiyo
News
Thursday, April 28, 2016
0 Response to "Serikali Kuwasilisha Mswada wa Sheria ya Ndoa"
Post a Comment