MSHAHARA WA RAIS WA TANZANIA KWA MUJIBU WA KATIBA YA 1977

blogger templates

Baada ya vuta nikuvute juu ya suala la mshahara anaolipwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, na kuibuka hadharani kutaja kiasi anacholipwa ambacho ni shilingi milioni 9.5 kwa mwezi.

Mara baada ya Dk. Magufuli kuweka bayana suala hilo kupitia Clouds 360 ya Clouds Televisheni, baadhi ya wabunge wa upinzani waliibuka na kumtaka ataje posho mbali na mshahara alioutaja.

Suala hilo limeibuliwa tena bungeni mjini Dodoma baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza (Chadema) kumuomba Rais John Magufuli kujipunguzia mshahara.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 43 (1), inasema Rais atalipwa mshahara na malipo mengineyo na atakapostaafu, atapokea malipo ya uzeeni, kiinua mgongo, posho, kadiri itakavyoamuliwa na Bunge na mshahara, malipo hayo mengineyo, malipo ya uzeeni na kiinua mgongo hicho, vyote vitatokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya serikali na vitatolewa kwa mujibu wa masharti ya ibara hiyo.

Ibara ndogo ya pili inasema mshahara na malipo mengineyo yote ya Rais havitapunguzwa wakati Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba


katiba mshahara wa Rais

0 Response to "MSHAHARA WA RAIS WA TANZANIA KWA MUJIBU WA KATIBA YA 1977"

Post a Comment