Mr Blue analalamika kuwa Sugu ameupora wimbo wake ‘Freedom’ aliokuwa
amemshirikisha kwa kutoa verse zake na kuufanyia video iliyotoka jana.
Lakini katika kila malalamiko, ni vyema kusikiliza pande zote
zinazohusika kwenye jambo husika ili kuupata ukweli. MJ Records
walioutayarisha wimbo huo wamezungumza kuelezea mambo yalikuwaje.
Producer mkuu wa studio hiyo, Marco Chali ameiambia Bongo5 kuwa beat ya
wimbo huo ilitengenezwa na mdogo wake, Daxo Chali aliyetengeneza chorus
yake na alimpa msanii wake Lizzy aliyeingiza. “Ngoma ilikuwa ipo tayari
na ilikuwa inasubiria verse tu kadhaa halafu ilikuwa ni ngoma yake
[Daxo]. Kwahiyo jamaa [Blue] akawa ameipenda tukampa akasema
atamshirikisha Mr Two,” amesema Marco.
Walipoifanya, Blue aliiamua kuiachia kupitia Mkito peke yake kwa maana
kwamba hakuiachia ngoma rasmi. Anasema baada ya muda Sugu alimpigia simu
kumuomba kuwa afanye version nyingine ya wimbo huo na aifanyie kabisa
na video.
Anadai alimuambia Sugu aongee na Daxo waliyekubali kuufanya tena hadi
video ikafanyika huku yeye [Marco] akiwa hajui chochote kilichoendelea
baada ya hapo. Na Marco anasema pia hakuhusika kwenye uingizaji wa sauti
zote mbili zaidi ya kuzifanyia mixing peke yake.
Marco amesema anadhani wawili hao [Sugu na Blue] waliongea kuhusu hatua
hiyo na kwamba wao kama studio hawakuwa na kipingamizi chochote kuhusu
kurudiwa kwa wimbo huo kwasababu walitaka wimbo ufike mahali.
Hata hivyo Marco amedai kuwa wote wawili [Sugu na Blue] hawakulipia
wimbo huo na kwamba MJ Records iliwapa kwasababu ya ‘love’ tu. Marco
anasema anashangaa kuona Mr Blue sasa hivi anatoa malalamiko hayo. “Ni
kwasababu mimi nilipenda tu kutoa studio bure kwanini usijitahidi
ukapeleka hiyo nyimbo ikafika sehemu ikafahamika, at least pia akili za
watu zilizotumika watu wazione. Na ndio hicho kitu naona ni kizuri, yeye
kwa mfano angefanya hata video, sidhani kama Sugu angerudia huo wimbo,”
ameongeza Marco.
entertaiment
Wednesday, April 27, 2016
0 Response to "Marco Chali: Wimbo wa 'Freedom' Sio wa Mr. Blue"
Post a Comment