Magufuli azua kizaazaa katikati ya jiji

blogger templates




maguuli


RAIS Dk. John Magufuli, jana alizua kiazazaa kwa wananchi wa maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam baada ya kuvamia Benki ya CRDB   akitumia gari lenye namba binafsi.
Kiongozi huyo wa nchi   alikwenda katika benki hiyo tawi la Holland akiwa kwenye gari lenye namba binafsi T 182 DFQ   likiwa halina nembo ya Adamu na Hawa wala bendera ya Rais.
Tukio hilo la aina yake ambalo lilichukua dakika 25, lilitokea asubuhi   katika tawi hilo ambalo liko katika makutano ya barabara za Ohio na Samora.
Baada ya Rais Magufuli kufika katika eneo liliko tawi hilo, barabara hizo zilifungwa ndipo aliposhuka kwenye gari hiyo aina ya BMW   na kuingia ndani ya benki hiyo.
Alipokuwa akikaribia kuingia katika benki hiyo,  baadhi ya wateja walijikuta wakikwama kuingia ndani ya benki hiyo baada ya  kuzuiwa na walinzi wa Rais huku huduma ikiendelea kwa wateja waliokuwa ndani.
Baada ya kuingia ndani baadhi ya wateja wa tawi hilo na wananchi wengine, walibaki wakishangaa huku wengine wakijiuliza ilikuwaje kiongozi huyo wa nchi   aingie ndani ya benki kwa staili ya aina yake likiwa ni tukio tofauti na marais waliomtangulia.
Mmoja wa wananchi waliokuwa jirani na benki hiyo ambaye alijitambulisha kwa jina la James Charles na ambaye ni dereva wa teksi, alisema baadhi ya wananchi waliokuwa kwenye eneo hilo baada ya kuona ulinzi unaimarishwa, walishtuka na mara wakamuona Rais Magufuli akishuka kwenye gari, hali iliyowafanya wafikirie anakwenda kutembelea ofisi yake ya zamani

0 Response to " Magufuli azua kizaazaa katikati ya jiji "

Post a Comment