Unafukuzia mwanamke mzuri mnaanza kuzungumza. Mnachukua muda wa dakika
20 hadi 30 kuongea na yeye mara ya kwanza. Anapendeza na kuvutia, na
unaona kama ni mwanamke ambaye ni yule aliyekuwa ndotoni mwako maishani
mwako. Mazungumzo yenu yanaenda vizuri mpaka ukwamwomba namba
yake
Baadaye unajaribu kumtumia text na hazijibu. Labda mnaeza kuchat kwa
madakika halafu baada ya hapa anakataa kujibu texts zako. Unabaki
ukijiuliza maswali ni kitu gani ambacho umefanya ambacho umekosea. Ok
labda anaweza kuwa yupo buzy unampa muda kiasi ajibu text
zako...unangojea masaa, siku, wiki mpaka inafikia wakati unagundua kuwa
amekupuuza. Kwa nini hajajibu text zako?
So kwa nini hakujibu text zako?
Katika situation nyingi ni kuwa sababu kuu ambayo amekataa kujibu texts
zako ni kuwa haukumpendeza mara ya kwanza ulipokutana naye. Ok labda
sababu nyingine inaweza ni kuwa ameibiwa simu yake wakati alipokuwa
akitext na wewe barabarani ama kitu kingine kama hicho, lakini hapa acha
tumakinike na hatua ya kwanza uliokutana naye...yaani first impression
ambayo unakudana na mwanamke yeyote.
1. Hakikisha unampendeza mara ya kwanza unapokutana naye
Anaweza kuwa hana muda mrefu wa kukaa na wewe ili akutambue zaidi so
kile kitu ambacho unahitaji kufanya ni kuwa lazima uuonyeshe upendo wako
kwa kuwa mpole, mkarimu na mtulivu. Hii itamfanya yeye kumakinika na
labda kutaka kukufahamu. Hakikisha kuwa wakati unapoongea na yeye tumia
mbinu za kuonyesha kuwa ungependa kukutana na yeye wakati mwingine. Kama
hakuonyesha dalili zozote za kukuelewa basi hata kama atakupatia namba
yake ya simu fahamu ya kwamba itakuwa ni kazi bure.
2. Taja sababu zako za kuongea na yeye
Mfano: Nimefurahia sana kuongea na wewe. Kusema kweli nimependa maonezi
yetu machache. Nataka kwenda lakini naonelea wikendi nitakutext tukutane
ili tuongee tena. Hapa utakuwa umeeleza ajenda yako kwake hivyo ukianza
kuchat na yeye baadae haitakuwa vigumu kwake kukujibu.
3. Hakikisha kuwa unamtumia text wakati ufaao
Ukiomba namba ya simu kwa mwanamke inamaanisha kuwa wewe umeonyesha
intrest kwake vilevile mwanamke akikupatia namba yake ya simu
inamaanisha kuwa labda itakuwa amependezwa na wewe. Lakini je, ni muda
upi unaotakikana hadi umtext mwanamke huyo.
Wanawake wanapenda kuona wanababaikiwa na kufukuziwa. So usijaribu
kumtext hapo hapo wakati amekupatia namba yake. Hakikisha umejibatia
shughli nyingi ili usahau kabisa kama uchukua namba kwa mwanamke. Masaa
mazuri ambayo yangekuwa sawa ya kumtext ni baada ya masaa 24 baada ya
kuchukua namba yake. Hii itamfanya mwanamke yeyote kujiuliza maswali ya
kwa nini umechukua muda mrefu kumtext. Itamfanya kuingiwa na maswali ya
kama: kwani hajapenda chat yangu? yuko na mwingine? nk. Ukichukua muda
huu mrefu hadi kumtext, itakuwa rahisi kwake kukujibi.
ONYO: Hakikisha ya kwamba haupitishi zaidi ya siku tatu kwani anaweza kukusahau kwa haraka ama kuona unampotezea wakati wake.
4. Kitu cha kuandika kwa text yako ya kwanza
Messages za kwanza ambazo utazituma kwa mwanamke zitachangia pakubwa
kuona kama wewe uko uko interesting ama unaboa. Unaweza kuuharibu mchezo
mzima kama iwapo utaanza kumtext na mambo ambayo hayana manufaa kwake.
Kile kitu unachohitajika kufanya hapa ni kuonekana hauna haraka na
ujaribu kutumia lugha za kirafiki. Mfano unaweza kujaribu kumtext swala
ambalo aliligusia kwa chat iliyopita. Labda aliongea kuhusu kwenda
shopping na nduguyake, so swali lakini linaweza kuwa: Je ile shopping
yenu na nduguyako iliendaje?. Hii itamfanya kuwa interested na wewe
manake ataona ya kuwa ulikuwa umemakinika wakati mlipokuwa pamoja. Hii
itamfanya kujibu text zako mara kwa mara bila yeye kuchoshwa.
5. Jaribu kuhepa stori ambazo hazitafikia popote
Mara ya kwanza anaweza kukujibu lakini itafikia pahali atanyamaza.
KUMBUKA: Siri kuu ya kumfanya mwanamke ajibu texts zako ni uwe makini
kwake, yaani unamtext vtu ambavyo unajua yuko intrested navyo.
6. Weka wazi kuwa unataka mkutano
Acha stori za kumzungusha huku na huku kama wanaume wengine. Ukitaka
akujibu text zako hakikisha ya kuwa unadhihirisha azma yako kwa
kumwambia kuwa unataka kukutana naye.
7. Usikate tamaa
Kuna wanaume wengine kama wamekataliwa kujibiwa texts zao mara moja basi
wanakasirika na wanaachana kabisa na kushungulika tena. Tatizo labda
linaweza kuwa mwanamke anakupima akili aone bidii yako kwake. Kama
tujuavyo tabia za wanawake ni kuwa hawapendi kuonekana kama ni watu wa
kukubaliana na kila kitu hivyo basi wakati mwingine wanakuwa
hawaeleweki.
Ukiona mwanamke amekataa kujibu text yako kwa siku tatu, fanya kumtext
tena huku ukionyesha kuwa hauna intrest naye sana vile halafu achana
naye. Hii itamfanya yeye kuona una interest na yeye lakini hauna haraka.
Baadaye anaweza kuanza chat yeye mwenyewe
KUMBUKA: Kuna sababu tofauti tofauti ambazo zinaweza kumfanya
mwanamke kukataa kujibu texts zako. Labda umemtusi, hujampendeza, ni
mwanamke mwenye haya nk. So hizi hatua zitategemea na vile imetokea
katika situation yako
entertaiment
Saturday, April 23, 2016
0 Response to "Hatua Za Kufanya Kama Mwanamke Hataki Kujibu Texts Zako"
Post a Comment