Daaah!!Nimejistukia tu na-tune Clouds Tv,nikakutana na kipindi cha "TAKE
ONE" cha Zamaladi,huyu mwanamke Faiza anayoongea yamenistua
Anasema yeye kuuza huwa anauza,huwa anajilipua ili mradi maisha yawe
vizuri.Anasema yeye sio kama wanawake wengine wanafiki wanaojidai
kupenda pasipo na pesa.Yeye hupenda mahali penye pesa na huwa hakai
kihasarahasara.Anasema aliwahi kuwa na bwana wa Kijerumani ambaye
walikuwa wanakutana Hong Kong kula bata,walikuja kuachana baada ya siku
Faiza kwenda na jamaa na washikaji zake Club ya usiku ambapo walikuta
mademu "wanaouza" na wanafahamiana na Faiza.Jamaa alipoona wale "malaya"
wanafahamiana na Faiza akaona hata Faiza atakuwa wa tabia hizo hizo.
Anasema yeye anajuwa kukaa sehemu ambazo atakutana na wanaume wenye hela
zao,na huwa hatoi tu kwa mwanaume kihasarahasara.Yaani hapo tu
anahojiwa kigauni alichovaa kila kaibadirisha mkao wa kukaa,mapaja wazi
mpaka watazamaji tumejuwa alikuwa amevaa "kufuri" nyeupe...Daah kweli
kuna watu fyatu kwenye hii dunia...Asalaleeeeee
Alipoulizwa kama anamsemaje Sugu mzazi mwenzake,akaanza kulia,anasema
anampenda sana Sugu,anakumbuka good time za Sugu,wakiwa wanabarizi na
kula bata huku na kule,na wakati wa msimu wa bunge alikuwa anamsindikiza
hadi Bungeni.Anasema anajuwa Sugu hampendi lkn yeye anataka Sugu ajuwe
huko aliko kuwa anampenda sana.
Anasema Sugu alimkuta akiwa na nyumba na gari mbili na biashara zake
ambazo alizipata kwa kujilipua sana ukiwemo hata kuuweka mwili wake
sokoni.
Anasema yeye ni Mama bora,na anamlea mwanae kisasa zaidi,na anasema
anamlea mwanae tofauti hata ya yeye alivyolelewa na Mama yake,anasema
anavyojiangalia yeye anatamani hata mama yake angemlea kama yeye
anavyomlea Sasha
Leo alikuwa anatangaza filamu yake mpya,ambayo ameomba watu wamuunge
mkono bila kujali tabia zake kwamba sijui alivaa "dippers" au siku ya
Zali's White Party alivaa kivazi cha kuwachanganya watu
News
Wednesday, April 27, 2016
0 Response to " Faiza wa Sugu Afunguka: Nilikuwa Nauza Mwili Kwa Faida..Bado Nampenda Sugu Nakumbuka Good Times"
Post a Comment