Daraja la kisasa kuzinduliwa Kigamboni

blogger templates

 Tanzania inatarajia kufungua daraja la Kigamboni ambalo kwa sasa ndilo daraja refu zaidi Afrika Mashariki linalobeba uzito kwa nyaya. Daraja hilo litaunganisha eneo la Kigamboni na Dar es Salaam.
Daraja hilo litafunguliwa rasmi na Rais John Pombe Magufuli kesho na kuunganisha mkondo wa Kurasini jijini Dar es salaam hadi eneo la Kigamboni.
Ujenzi wa daraja hilo umegharimu zaidi dola milioni 140, na litachukua nafasi ya feri inayosafirisha watu na magari kati ya Kigamboni na kivukoni upande wa Dar es Salaam.

0 Response to "Daraja la kisasa kuzinduliwa Kigamboni"

Post a Comment