CUF: SERIKALI YA MAGUFULI INAUA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

blogger templates

Hakuna asiye fahamu umuhimu wa vyombo vya habari katika jamii kwani vinamchango mkubwa katika maendeleo ya taifa, majuma kadhaa yaliyopita waziri mwenye dhamana ya kusimamia tasnia ya habari nchini Nape Nnauye alitangaza mabadiliko katika urushwaji wa matangazo ya bunge kupitia Luninga ya Taifa TBC, ambapo alisema halitakuwa la moja kwa moja kutokana na gharama za uendeshaji.

Je kuna umuhimu wowote wa kurusha matangazo ya bunge moja kwa moja?, jibu la swali hilo analo Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chama cha Wananchi CUF Abdul Kambaya, ambapo katika Mkutano wake na Waandishi, leo jijini Dar es Salaam ameeleza kuwa bunge likirushwa moja kwa moja linaongeza uwajibikaji, uwazi hivyo kutolionesha moja kwa moja ni kinyume na sheria ya Uhuru wa Habari kifungu cha 18 katiba ya mwaka 1977.

Naibu Mkurugenzi huyo amesikitishwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuvinyima uhuru vyombo binafsi vya habari katika kuripoti habari za bunge kwani amesema kuwa Bunge limeanzisha kituo chake cha kurusha matangazo ambapo wanahabari watakuwa wanapatiwa habari na chombo hicho, pia hairuhusiwi kwa muandishi kuingia na kamera au kinasa sauti bungeni jambo ambalo amelifananisha na udikteta.

Kutokana na hayo Naibu Mkurugenzi wa Habari Kambaya amesema kuwa chama chake cha CUF kipo tayari kushirikiana na vyombo vya habari binafsi kupambana kufanikisha kuwa Uhuru wa vyombo vya habari unapatikana kwani gharama za uendeshaji sio sababu ya msingi akidai kuwa luninga ya Taifa inapata ruzuku ya serikali inayo tokana na kodi za wananchi, hivyo isiwe kisingizio cha kuwaficha wananchi ili madudu ya serikali yapite bila kupingwa.

0 Response to "CUF: SERIKALI YA MAGUFULI INAUA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI"

Post a Comment