MUME wa mwanamke anayedaiwa kumkamata ugoni Askofu Dk Alex Malasusa wa
Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania (KKK) Dayosisi ya Mashariki na
Pwani, (DMP) anatafuta watoto waliotoroshwa kwa maelekezo ya Malasusa na
Jeshi la Polisi, anandika Josephat Isango.
Akizungumza baada ya kuachiwa huru kutoka polisi kwa tuhuma za
kushambulia, amesema watoto wake walichukuliwa na raia mmoja mjerumani
aliyeolewa na mtanzania, anaitwa Caroline Shedafa.
Caroline Shedafa ametuhumiwa kuwa ametumia mwanya wa malalamiko ya
Mwakilima na Malasusa kwa sababu ya urafiki alifanikiwa kuwatorosha
watoto hao na kwamba ana mpango wa kuwasafirisha kwenda nje ya nchi
wakati wowote.
MwanaHALISI limemtafuta Shedafa kwa tuhuma hizo, alipokea simu na baada
ya kuambiwa kuwa anaongea na MwanaHALISI alikata simu na kukataa kuongea
suala hili na mwandishi.
Malasusa anadaiwa kuwa anadaiwa kushirikiana na mfanyakazi wa hospitali
ya Muhimbili anayeitwa Julieti, aliyewaambia ndugu wa mume
anayenyang’anywa mke wake na malasusa kuwa atakiona.
“Huyu kaka anajidai mjuaji, hapti kitu, utaratibu uko tayari wa
kuwasafirisha watoto kwenda nje ya nchi na hatawaona tena, ataishia
kuwasikia tu, mimi ni mtu wa Karibu na Askofu Malasusa ndo nawaambia”.
Alinukuliwa dada huyo akiongea kwa ujasiri.
Hadi sasa watoto wanaotafutwa na baba yao ambao Jeshi la Polisi
linadaiwa kushirikiana na Malasusa licha ya taarifa zao kufika polisi
kituo cha Wazo na kutochukuliwa hatua ni Sijenuni, Sephania, na Simon
wote wanadaiwa kuwa watoto wa Venance Mwakilima.
Taarifa za leo usiku zilizofikiwa MwanaHALISI online zinadai kuwa baadhi
ya Maaskofu Jijini Dar es Salaam wameamua kujitokea kulinda heshima ya
uaskofu baada ya kudhalilishwa na Malasusa.
Maaskofu ambao hawakupenda kutajwa majina yao kwa kuwa si wasemaji wa vikao halali wamesema “hili suala tunalichukua,
Malasusa ana tuhuma nzito nchini, na baada ya gazeti kuandika watu
wamejitolea kujieleza tunaomba muda kesho (Jumanne) tutaliongelea
hadharani baada ya kukutana na mume wa me.
Aidha Malasusa hakupatikana kwenye simu zake wala kujibu ujumbe wa simu
aliotumiwa tangu juzi wakati gazeti la MwanaHALISI likiendelea
kufuatilia sakata hili.
Taarifa ambazo mwandishi anazo zinadai viongozi wakubwa wa serikali
wanaingilia suala hili, zinafuatiliwa na zitaandikwa kwenye gazeti la
MSETO…
News
Monday, April 25, 2016
0 Response to "BAKING NEWS:Askofu Dr Malasusa wa (KKK) Akamatwa Ugoni"
Post a Comment