CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya
Rorya mkoani Mara kimesema watu wanaokejeli juhudi zinazofanywa na Rais
John Magufuli si wazalendo , wanapaswa kuchunguzwa na Serikali.Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Rorya, Samwel Kiboye alisema hayo jana jijini Mwanza
alipokuwa akizungumzia juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli kuchukua
hatua dhidi ya watu wanaoiba fedha za umma.
“Kumeibuka tabia chafu kutoka kwa
baadhi ya watu nchini kwa sasa, wanapotosha wananchi juu ya kazi nzuri
inayofanywa na Rais Magufuli katika kuwashughulikia mafisadi na wanaoiba
rasilimali za nchi, ”alisema.
Alisema taifa haliwezi kukubali kuona
kazi nzuri inayofanywa na Rais ikipotoshwa na watu wachache aliosema
hawaitakii mema nchi. “Nani haoni kazi kubwa inayofanywa na Rais …,
ameimarisha ukusanyaji wa mapato na ameboresha sekta ya afya,
miundombinu, hivi watu hawa wanataka Rais awafanyie nini?,” alihoji na
kuongeza:
“Ni aibu kuona watu wanahoji mambo
ambayo hata kwa mtu ambaye hakwenda shule anaona mafanikio makubwa
aliyofanya Rais Magufuli katika kipindi kifupi ambacho amekuwa
madarakani.”
“Huko nyuma walikuwa wanamlaumu
aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne Jakaya Kikwete kuwa alikuwa mpole, leo
tumempata Rais anayesimamia ukuaji wa uchumi wa nchi wanaleta siasa,
sisi Rorya tunasema tuko imara na tutakufa na Rais Magufuli”
0 Response to "ATAKA WANAOKEJELI JPM WACHUNGUZWE"
Post a Comment