Afisa uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara Bw.
Julius Bujabhi Makwasa amehukumiwa kifungo cha Miaka 7 jela baada ya
kupatikana na hatia ya Makosa 34 yakiwepo ya Rushwa.
Mnamo mwaka 2013 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Mara
ilimfikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Serengeti Afisa uchaguzi wa
Halmashauri hiyo Bwana Julius Bujabhi Makwasa na wenzake wawili
wakishitakiwa kwa makosa thelathini na manne yakiwemo ya matumizi mabaya
ya fedha za umma, kuisababishia hasara Halmashauri ya Serengeti,
kusaidia kutenda kosa, kughushi na kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri
wao.
Washitakiwa wengine katika shauri hilo la uhujumu Uchumi E.C.C 130/2013
lililokuwa likisikilizwa na Hakimu wa Mahakama hiyo Mheshimiwa Ismail
Emanuel Ngaile, walikuwa Bi Scola Daudi Mosi ambaye ni mtunza
kumbukumbu wa Halmashauri hiyo na Bwana Dickson Julius Makwasa ambaye ni
mtoto wa mshitakiwa wa kwanza.
Ilidaiwa na mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Wakili Martin Makani mbele
ya mheshimiwa Ngaile kwamba mshitakiwa wa kwanza Julius Makwasa ambaye
majukumu yake yalikuwa pamoja na kuviteketeza vifaa vya uchaguzi muda wa
uchaguzi unapopita na mshitakiwa wa pili Scola Mossy ambaye majukumu
yake ni pamoja kusimamia kumbukumbu zinazoingia na zinazotoka nje ya
Halmashauri hiyo, kwa nafasi zao hizo, walikuwa na jukumu la kuharibu
nyaraka za uchaguzi mkuu wa Octoba 2010 kama ilivyokuwa imeelekezwa na
Tume ya Taifa ya uchaguzi.
Katika kutekeleza jukumu hilo ilielezwa kwamba, waliandaa majina ya
vibarua na kuingiza majina hewa ishirini na tano (25) kuonyesha kwamba
majina hayo hewa pia yalishiriki kuchimba mashimo, kusomba nyaraka hizo
za uchaguzi na kuzipeleka kwenye mashimo kisha kuziteketeza kwa moto
hivyo kustahili malipo.
Katika udanganyifu huo ilielezwa kwamba, mshitakiwa wa kwanza na wa pili
waliweza kuandaa nyaraka za kuipotosha Halmashauri ya Wilaya ya
Serengeti na kuwawezesha kujipatia jumla ya shilingi million tatu laki
nane na elfu hamsini (Tsh 3,850,000/=) kwa kutumia nyaraka kumdanganya
mwajiri
News
Monday, April 25, 2016
0 Response to "Afisa Uchaguzi ahukumiwa kifungo cha Miaka 7 jela kwa Rushwa"
Post a Comment